Tuesday, 24 January 2017

BAGAMOYO: MJI WENYE SIFA ZA KIPEKEE


Bagamoyo ni mji ulioanzishwa mwishoni mwa karne ya 18. Ukiwa kama mji mkuu wa Wajerumani Afrika Mashariki, mji ulio kua na bandari kubwa na biashara nyingi wakati ule.

Hapo awali kabla yakufikia karne ya 18, bagamoyo ilikua ni kituo kidogo cha biashara mbalimbali ikiwemo samaki, chumvi na gundi. wakazi wake wengi walikua ni wavuvi wa samaki na wakulima.

Katika karne ya 19, waarabu waliwasili na kupageuza kua kitovu cha biashara ya utumwa kwa Afrika Mashariki. Hii ilipoteza sifa yake iliokua nayo kwa kiasi kikubwa kwani walipageuza kua ndio kituo cha misafara ya watumwa kutoka katika ya nchi. 

Mwishoni mwa karne ya 18 familia 12 za kiislam ziliweka makazi katika mji wa bagamoyo wakiwa wote ndugu wa Shamvi La Magimba kutoka Oman. walio ishi kwa kulazimisha makusanyo ya kodi kwa watu hata kwenye mambo kama kuchinja mbuzi au kuvua samaki, na biashara ya chumvi, ambayo ilikua inafanyikia vijiji vya Nunge, umbali wa KM 3 kaskazini mwa Bagamoyo.

Watumwa walikua wakiwekwa katika magereza na inapofika usiku, walikua wakisafirishwa kwa meli katika soko la wa tumwa mjini Zanzibari. Hii ilitengeneza maana ya jina BAGAMOYO(Bwaga-Moyo). Kwamba wale walio kua wakisafirishwa kutoka Bagamoyo walikua hawarudi tena nyumbani kwao.

sanamu zikionyesha jinsi gani watumwa walikua wanafungwa wakisubiri kusafirishwa kwenda kuuzwa zanzibari.


Mwaka 1868: kulianzishwa kwa misheni ya kikatoliki
Katika mwaka 1868, watawala wadogo mjini Bagamoyo walio julikana kama wajumbe, waliwasilisha misheni (dini) ya kikatoliki (mababa wa roho mtakatifu) jambo lililoleta upinzani kutoka kwa watu wenye asili ya kizaramo ambao walikua wakiongozwa katika misingi ya Sultani Majid na baadae mwaka 1870 Sultan Barghash.

misheni (kanisa) lililotumiwa na viongozi wa kikatoliki kuhifadhi watoto walio nusurika katika bisahara ya utumwa, pia walipatumia kwa kusalia, na kufundishia.



Awali misheni hii ilianzishwa kwa lengo la kuwahifadhi watoto walio okolewa katika biashara ya utumwa, lakini baadae ilikua kubwa na kugeuka kua kanisa, shule na sehemu ya kufanyia kazi za mikono pamoja na shuguli za kilimo.

Bagamoyo ndio mji pekee kutembelewa na watafiti wa kwanza kutoka mabara ya ulaya Katika karne ya 19, ambapo ilikua ndio mwanzo kwa misafara ya Livingstone na wengine. Kwani mji wa Bagamoyo Haukuwa tu kituo cha biashara kwa ajili ya watumwa na bidhaa za biashara (pembe za ndovu au Nguta, ambayo ilivunwa kutoka katika nazi na ilitumika kwa ajili ya utengenezaji wa sabuni) au kituo cha kutengeneza mashua, lakini ulikua ndio mwanzo wa ujio wa wavumbuzi na watafiti kutoka ulaya.

Walikua wakitoka nje ya mji wa Bagamoyo wakitafuta chanzo cha ziwa Nile na maziwa mengine amabyo yalikua hayaja gunduliwa kwa wakati ule.  


Kati ya walioanza safari yao kutoka Bagamoyo alikua ni livingstone, burton, speke ambao walikwenda pamoja na Grant kutatua siri za chemchem za mto Nile. Grant pamoja na Stanley ambao walivunja uhusiano wao katika miaka ya 1871 na mabaharia 192 na tani 6 ya vifaa, katika kusaka Livingston iliopotea. Na baadaye tena mwaka 1889 wakati yeye anarudi kutoka miaka 3 ya msafara na wafanyakazi wake, idadi ilikua imepungua kutoka 708 mpka 196.

Bagamoyo pia ikawa maarufu kupitia kurudi kwa Livingstone: Baada ya safari ya miezi 9 kutoka Zambia, msiidizi wa livingstone kutoka zanzibari Abdullah Susi na James Chuma walileta maiti yake ilio kaushwa mjini Bagamoyo mwezi wa pili mwaka 1874.

Mji wa Bagamoyo unajivunia kuwa na makabila mbalimbali ikiwemo Zaramo na Doe, Shomvi Waislamu kutoka Oman, hindu kutoka India pamoja na waislamu wengine kutoka Zanzibari. ambao kwa pamoja wanaishi kwa amani na ushirikiano katika maisha ya kila siku. 


Bagamoyo umekua kivutio kikubwa sana kwa watalii kutoka nje ya nchi kutokana na maajabu mengi au historia kubwa ilio kua nayo katika suala ya watumwa pamoja na uanzilishwaji wa udini. 

Mji ambao umezungukwa na hoteli kubwa na za kifahari kwaajili ya wattalii, wageni pamoja na wazawa ambao wangependa kuchukua nafasi kuitembelea na kujifunza mambo mengi ya nyakati za kale kama sehemu moja wapo ya kujua jinsi gani wazee wetu wa zamani waliishi. 

Hatahivyo mji wa Bagamoyo unabaki kua na sifa nyingi za kipekee ambazo miji mingine yeto haikubahatika kuanazo jambo linalo gusa nyoyo za watalii wengi na kuifanya kua kivutio kikubwa kwa watu wengi. 

No comments:

Post a Comment